.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
15
Mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa
 kesi za mauaji wameleta kizaazaa baada ya kujaribu
 kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa na
 kuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu. Tukio hilo
 limetokea May 7 2014 saa nne asubuhi katika

 Mahakama ya Hakimu 
Mfawidhi wa Wilaya ya
 Nyamagana Mwanza walipofikishwa kwa ajili ya
 kusikilizwa kwa kesi zao lakini ghafla walipofika kwenye
 viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbio
 kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya
 Taifa na kuvua nguo kisha kuanza kupiga
 kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke. 
Ni Thobiasi Warioba (35) alieamua kuvua nguo zote na
 kubaki mtupu eneo la mlingoti wa bendera ya taifa,
 ambaye anakabiliwa na kesi ya
 mauaji Na. 32/2012. Watuhumiwa wengine 
waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35),
 Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine
 ambaye hakufahamika majina
 yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013 na
 walikamatwa tangu mwaka 2011.
 13 Baada ya kudhibitiwa na askari polisi walisikika wakisema:
 “haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi
 sasa kesi zetu hazijasikilizwa, wengine tumebambikiziwa
 kesi tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya
 habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila
 kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011
 tulipokamatwa, tumechoka kukaa mahabusu 
tunaomba kesi zetu zisikilizwe”. Baada ya malalamiko 
yao askari mmoja aitwae Inspekta Henry akiwa n
a wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie
 aliwahoji kuhusiana na madai yao huku askari hao wakiwataka
 kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka
Warioba avae nguo ili waweze kuingia Mahakamani. 
15Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya 
Tanzania Kanda ya Mwanza ambae alikataa kutajwa
 jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao
 bado haujakamilika na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa
 na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake 
zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu. 17 16
 SONY DSC 18Unataka stori kama hizi zisikupite? jiunge
 na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo
 la @millardayo na nitakua nakutumia stori kama hizi kila zinaponifikia.

0 comments:

Post a Comment