.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |




Posted by kifesi |
Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni.

CCM na EATV(East Africa Television) Wameandika kwenye twitter yao.



By Kibo10:
Historia Fupi ya Marehemu John Komba

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Chanzo
: BBC
Posted by kifesi |
My Birthday wish for you is that you continue to love life and never stop dreaming. May beauty and happiness surround you not only on your special day, but always.

Posted by kifesi |

Words alone are not enough to express how happy I am you are celebrating another year of your life! My wish for you on your birthday is you are and will always be happy and healthy! Don’t every change.

Posted by kifesi |
MTI4MzA5MDkyMDk4ODMwMzA2
Lupita Nyong’o alikuwa mmoja ya wanamitindo na mastaa ambao walipendezesha Red Carpet na event yote ya sherehe za Tuzo za Oscars mwaka huu ambazo zilifanyika siku ya Jumapili February 22 Marekani.
Kuanzia siku ya jana kuna story ambayo ime hit vichwa vya habari vingi kuhusu Lupita, lile gauni lake kali ambalo alivaa siku ya event hiyo limeibiwa katika chumba cha Hotel ambayo alikuwemo staa huyo.
Thamani ya gauni ni dola 150,000/-, sio hela ndogo kiukweli, ni kama mil. 270 Tshs.
Gauni hilo lilikuwa maalum kwa ajili ya Lupita, lilitengenezwa na Calvin Clain.
lupita-nyongo-2015-oscars-arrival-02
Hotel hiyo ya London Hotel iliyopo 
Hollywood
 wamesema kuwa wanashirikiana na Polisi kufanya upelelezi kukagua picha za kwenye  camera ya CCTV, wanaamini aliyeiba atapatikana kwa kuwa kama mtu alitoka amelibeba lazima wataweza kumgundua kutokana na ukubwa na uzito wa gauni hilo.

Chumba cha Lupita kilikuwa busy kutokana na watu wengi kuingia humo ikiwemo watu wa mitindo, make up, mameneja na marafiki zake wa karibu pia.
Posted by kifesi |

Likija swala la fashion na kuvaa kulingana na wakati Miss Temeke huwa hakosei,sasa basi katika  picha ya kwana ni binti wa superstaa Kevin Costner' alivokua amevaa at 'Black or White' Movie Premiere @Hollywood the same dress alovaa Miss T siku ya valentines,we unahis nani alifunikaa
Posted by kifesi |
Posted by kifesi |




Posted by kifesi |







Posted by kifesi |

Ili uwe na ndoa furaha,kamwe usiolewe na mwanamme asiempenda Mama ake na usioe mwanamke
 ambae hakua Good daughter
Posted by kifesi |
Click image for larger version. 

Name: Gold.jpg 
Views: 0 
Size: 15.9 KB 
ID: 230161
Ili dhahabu iweze kung'aa na kuwa na thamani zaidi lazima ichomwe moto, ipitishwe kwenye tanuru la moto. Wale wasomaji wa vitabu vya dini kunasehemu imeandikwa " Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji."

Kuna mambo hapa ni lazima kuya elewa "Nijapo pita kati ya bode la uvuli wa mauti. Hapa ni kupita katika hali inayokufanya ujisikie kutokuwa na thamani, hali ngumu lakini lengo lake ni wewe kuwa safi ili uweze kuifikia hiyo ndoto yako na kuitumikia vyema.

Nelson mandela alikuwa na ndoto ya kufikia kitu fulani. Ilimchukua hatua fulani mpaka kufikia hiyo ndoto yake. Yusufu naye japo kuwa alioa kuwa ndugu zake watamwinamia na kumpigia magoti. Haikuweza kutokea wakati huo huo tu.

Ni lazima kupitia "process" ili ukamilike. Na kuna asilimia kubwa ya watu wanashindwa mitihani. Ndio maana unakuta wanarudia rudia hatu hiyo. Katika kuelekea ndoto hakuna njia ya mkato ni lazima ukamilishe mafunzo na uwe kamili.

Kuna watu wapo kabisa kwa ajili ya kukuweka uwe "pure" watakuchoma, watakupika, watakupiga na watakutesa. Lengo lake ni kufikia ndoto "
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika" Watesi wapo kabisa tena kwa nia nzuri kwako ili uweze kung'aa na kuongeza thamani yako.

Mtoto mjinga ataanza kulia na kumsumbua mama yake kuwa ampe chakula, wakati maama anaosha mchele ili apike wali tena na nyama ya kuku ili vikiivya mtoto wake ale afurahi. Toto jinga litasumbua litalia mpaka litachoka na kulala bila hata kula huo wali na nyama ya kuku. Lakini mtoto mwenye busara husubiria na kukaa karibu na mama yake huku akimuuliza "mama leo unanipikia wali na kuku". Mama humjibu majibu mazuri na mtoto husubiri baadae hula na kufurahi.

Ndivyo hivyo kuelekea kwenye ndoto. Watu hukutana na changamoto ndogo tu ya njaa na kukata tamaa kabisa. Hatimaye kuwa watu wabaya, wezi na wanafanya mambo yafananayo na hayo. Wanashindwa kuvumilia na kujua kuwa kila kitu lazima kipitie kwenye "Process".

Huwezi ukajikuta tu eti sasa hivi upo mwanza lazima kunahatua utakazo zifanya zingine zinachosha lakini kwakuwa mpango wako ni kwenda mwanza utavumilia na hatimaye safari itaanza na utafika mwanza.

Ndoto yako unaweza ukaichelewesha kwa kuwa ni mgumu kuelewa somo au usiifikie kabisa. Ni kama toto lile jinga. Mama anaweza akaahirisha kabisa kupika na kuanza kulishughulikia.
Posted by kifesi |
JINA la Zari hivi sasa limekuwa jina maarufu katika masikio ya Watanzania, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya mwanadada huyo mfanyabiashara na mwanamuziki wa Uganda kuwa na urafiki na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kwa jina la usanii Diamond Platnum.
Zari The Lady Boss
Kwenye mitandao ya kijamii kama Tweeter, 
Facebook
,Instagram na hata Whatsapp lazima utakutana na jina Zari akiunganishwa na Diamond na wengine wataunganisha na Wema Sepetu aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Uhusiano kati ya Zari na Diamond umezua gumzo kila eneo Tanzania na Afrika Mashariki huku wakifananishwa na mastaa wa nje kama vile 
Kanye West
 na 
Kim Kardashian
 kwa namna wanavyofuatana wakati wote huku Diamond akionesha kila aina ya mbwembwe za kumjali mrembo huyo kutoka Kampala, Uganda.

Uhusiano wa Zari na Diamond umewafanya kuandamana kila sehemu hivi sasa. Wawili hao walianza kuonekana kuwa na ukaribu wa mahusiano tangu Diamond alipokwenda Afrika Kusini kwenye Tuzo za Channel O ambapo Diamond aliibuka na ushindi wa Tuzo tatu.

Baada ya Tuzo hizo, Zari alimualika Diamond kushiriki katika ‘pati’ maarufu ambayo mwanadada huyo huandaa kila mwaka nchini Uganda ambapo mwaka huu ilijulikana kama All White Ciroc Party.

Wawili hao baada ya sherehe hiyo, walifuatana ambapo Zari alimsindikiza Diamond nchini Rwanda na Burundi alipokwenda kutoa burudani nchini humo, na picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kuwafanya wawili hao kuwa gumzo hivi sasa katika mitandao Tanzania na Afrika Mashariki.

Je, Zari ni nani hasa? Zarina Hassan Tlale.Maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini.

Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006,Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports .

Mwanadada huyo ni binti wa Halima Sultan Hassan na Nasur Hassan akiwa na asili ya damu mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ya Kihindi , Toro, Somalia na Burundi kutoka mji wa Jinja, Uganda. Babu mzaa mama yake anatoka India na bibi yake ni kutoka Uganda. Babu yake mzaa baba ni kutoka Somalia na bibi yake mzaa baba anatoka Burundi.

Zari maarufu kama The Bosslady aliwahi kuolewa na mwanamume anayejulikana kwa jina la Ivan na kubarikiwa watoto watatu wa kiume Pinto, Didy na Quincy na anamiliki kampuni tatu.

Mwanadada huyu alizaliwa Septemba 23,1980. Zari amekulia katika mji wa Jinja katika nchi ya Afrika Mashariki inayojulikana kama Uganda.

Zari alisoma shule ya msingi, kisha kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja ambapo alisoma kwa bidii kutimiza ndoto zake. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, mwanadada huyo alihamia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala ambapo alikuwa akitoa burudani ya muziki katika maeneo ya starehe kabla ya kuhamia mjini London, Uingereza na kusomea Stashahada ya masuala ya urembo (cosmetology).

Historia yake kimuziki inaonesha Zari alianza kuimba akiwa na umri mdogo wakati akisoma shule ya msingi ambapo alikuwa akitoa burudani katika matamasha ya muziki yaliyokuwa yanaandaliwa na wafanyakazi wa shule,wakati wa hafla za mwishoni mwa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya akiwakilisha shule yake.

Ingawa amekulia katika familia ya Kiislamu yenye wasichana sita na wavulana wawili, Zari hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Alianza muziki akiwa na umri mdogo na albamu yake ina nyimbo kali kama ‘Toloba’ na ‘Hotter Than Them’. Watu waliomvutia katika muziki ni Wasanii wa Marekani Arethal Franklin na Whitney Houston wakati akiwa sekondari.

Afrika waliomvutia akapenda muziki ni wanamuziki wa Afrika Kusini Brenda Fassie, Miriam Makeba, Lucky Dube na Malkia wa Muziki Afrika Kusini, Yvone Chaka Chaka. Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi,drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.

Baada ya miaka miwili ya kufanya vizuri katika majukwaa na matamasha ya shule, alipumzika na kuhama kutoka Uganda kwenda London, Uingereza na kuendelea na masomo yake lakini bado mapenzi yake kwa muziki yakiwa mawazoni mwake. Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .

Mwaka 2008 Zari alishinda Tuzo ya Channel O ya Video Bora ya Muziki ya Msanii Bora Afrika Mshariki. Hafla ya tuzo hizo ilifanyika Johannesburg, Afrika Kusini. Tangu hapo Zari ameendelea kutoa nyimbo zaidi za kuvutia, huku akitiwa moyo na mashabiki wake wakati huo.

Mwaka 2009 alipata Tuzo inayojulikana kama Diva ya mwaka katika kipengele cha Diaspora tangu hapo aliendelea kutengeneza muziki. Zari hivi sasa anaishi Afrika Kusini ambapo anamiliki maduka makubwa ya vipodozi na shule ya elimu ya juu mjini Pretoria wakati akiendelea kujijenga kimuziki.

Inaelezwa kuwa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan wanamiliki Shule ya Brooklyn City ambayo ina kampasi sita Afrika Kusini, huku kila moja ikiwa na wanafunzi kati ya 800 hadi 2,100. Wanafunzi hao hupewa vyeti vya taifa wanapomaliza mwaka. Vile vile Zari amejenga hosteli iliyopo barabara ya Sir Apollo Kaggwa, Kampala na anamiliki nyumba kadhaa katika mji huo hasa eneo la Munyonyo, pamoja na duka kubwa la nguo Afrika Kusini.

Ingawa muziki wake haujafanya vizuri kama wanamuziki wengine wa Uganda akiwemo Jose Chameleone, Bebe Cool, Bobi Wine na Ragga Dee, Zari amekuwa akifurahia kwa mafanikio zaidi kwenye biashara na kutokana na hilo anasema lazima arudishe kwa jamii na hivyo kuamua kusaidia vituo na taasisi kadhaa zinazohitaji misaada kama Katalemwa Cheshire Home, Sanyu Babies’ Home pamoja na Gereza la Luzira.

Mfano mwaka 2013 kutokana na moyo wake wa kusaidia,kwa kutimiza hilo baada ya sherehe zake anazozifanya kila mwisho wa mwaka aliamua kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha M-Lisada kilichopo Nsambya siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi, akifuatana na watoto wake Pinto, Didy na Quincy.

Alitoa zawadi maalum kwa watoto hao, ambapo Zari alishiriki kuandaa chakula cha Krismasi na kisha baadaye wanawake, sukari, biskuti, mchele na matoke. Mbali na masuala mengine yote, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,watu wengi nchini Uganda wanakubaliana kuwa Zari ndio Mwanamke Mrembo zaidi nchini humo.

“Sitafuti umaarufu, wenyewe umaarufu ndio hunifuata,”aliwahi Zari kusema kupitia mtandao wa Red Pepper akikanusha habari za baadhi ya watu wanaodai kuwa anatafuta umaarufu kwa nguvu.

Habari zake kuandikwa katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zake za uhisani zimesababisha wengi kudai kuwa anataka tu umaarufu, kujulikana na kuzungumziwa kila wakati.Hata hivyo akijibu madai hayo, Zari alisema umaarufu unamtafuta yeye na sio kwamba yeye anautafuta.
Posted by kifesi |
SAMSUNGtaarifa kutoka Nairobi Kenya ambayo ilisikitisha sana ni tukio la watoto watatu kuuawa na mwanamke mmoja ambaye baada ya kuwaua halafu akawapasua na kula mioyo ya watoto hao.
Mwanamke huyo Catherine Muthoni alimuua mtoto wake mmoja mwenye umri wa miaka kumi na baadaye kuua watoto hao wawili wa jirani.
Tukio la leo katika eneo la makaburi ya Lang’ata limewatoa wengi machozi wakikumbuka jinsi watoto hao walivyofariki kwa mateso ambapo familia ya watoto hao wameamua kufanya mazishi ya watoto wote wawili kwenye kaburi moja
Posted by kifesi |
CHINIItukio la kuanguka kwa mwanamuziki mkongwe Madonna limezungumziwa zaidi, hii imetokea bahati mbaya wakati mwanamama huyo akifanya show na dancers wake kwenye stage.
Posted by kifesi |
Posted by kifesi |
 Happy anniversary to the man I want beside me every night for the rest of forever. I love you Mohammed...........Alhamdulillah RabilaAllamina Mwenyezi Mungu nakushukuru kwa kutimiza miaka 13 Ya ndoa yetu.M/Mungu nakuomba uzidi kuniwekea Mume WANGU na umuepusha na maradhi,shari na husda za dunia.Eeeeh Yarabi nanyanyua mikono yangu uzidi kutulinda na ndoa yetu............... Ahsante sana mume wangu umenikuna panaponiwasha