.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
Click image for larger version. 

Name: Gold.jpg 
Views: 0 
Size: 15.9 KB 
ID: 230161
Ili dhahabu iweze kung'aa na kuwa na thamani zaidi lazima ichomwe moto, ipitishwe kwenye tanuru la moto. Wale wasomaji wa vitabu vya dini kunasehemu imeandikwa " Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji."

Kuna mambo hapa ni lazima kuya elewa "Nijapo pita kati ya bode la uvuli wa mauti. Hapa ni kupita katika hali inayokufanya ujisikie kutokuwa na thamani, hali ngumu lakini lengo lake ni wewe kuwa safi ili uweze kuifikia hiyo ndoto yako na kuitumikia vyema.

Nelson mandela alikuwa na ndoto ya kufikia kitu fulani. Ilimchukua hatua fulani mpaka kufikia hiyo ndoto yake. Yusufu naye japo kuwa alioa kuwa ndugu zake watamwinamia na kumpigia magoti. Haikuweza kutokea wakati huo huo tu.

Ni lazima kupitia "process" ili ukamilike. Na kuna asilimia kubwa ya watu wanashindwa mitihani. Ndio maana unakuta wanarudia rudia hatu hiyo. Katika kuelekea ndoto hakuna njia ya mkato ni lazima ukamilishe mafunzo na uwe kamili.

Kuna watu wapo kabisa kwa ajili ya kukuweka uwe "pure" watakuchoma, watakupika, watakupiga na watakutesa. Lengo lake ni kufikia ndoto "
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika" Watesi wapo kabisa tena kwa nia nzuri kwako ili uweze kung'aa na kuongeza thamani yako.

Mtoto mjinga ataanza kulia na kumsumbua mama yake kuwa ampe chakula, wakati maama anaosha mchele ili apike wali tena na nyama ya kuku ili vikiivya mtoto wake ale afurahi. Toto jinga litasumbua litalia mpaka litachoka na kulala bila hata kula huo wali na nyama ya kuku. Lakini mtoto mwenye busara husubiria na kukaa karibu na mama yake huku akimuuliza "mama leo unanipikia wali na kuku". Mama humjibu majibu mazuri na mtoto husubiri baadae hula na kufurahi.

Ndivyo hivyo kuelekea kwenye ndoto. Watu hukutana na changamoto ndogo tu ya njaa na kukata tamaa kabisa. Hatimaye kuwa watu wabaya, wezi na wanafanya mambo yafananayo na hayo. Wanashindwa kuvumilia na kujua kuwa kila kitu lazima kipitie kwenye "Process".

Huwezi ukajikuta tu eti sasa hivi upo mwanza lazima kunahatua utakazo zifanya zingine zinachosha lakini kwakuwa mpango wako ni kwenda mwanza utavumilia na hatimaye safari itaanza na utafika mwanza.

Ndoto yako unaweza ukaichelewesha kwa kuwa ni mgumu kuelewa somo au usiifikie kabisa. Ni kama toto lile jinga. Mama anaweza akaahirisha kabisa kupika na kuanza kulishughulikia.

0 comments:

Post a Comment