.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
Jeshi la Polisi linawahoji watu nane wakiwemo Madaktari wa chuo cha kitabibu cha IMTU kwa madai ya kutupa mabaki ya masalia ya binadamu katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji kata ya Mbweni wilayani Kinondoni Dar es salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.
‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova
Screen Shot 2014-07-24 at 3.44.25 AMKwenye hii ishu pia hospitali ya taifa Muhimbili inachunguzwa ambapo mkuu wa kitengo cha uhusiano kwenye hospitali hii ya taifa Aminiel Aligaesha amesema >> ‘Sisi ni miongoni mwa wanaochunguzwa kwa sababu ni hospitali mojawapo katika jiji la Dar, mabaki yale hayakutoka hospitali ya taifa Muhimbili’
‘Kuharibika kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea kuitengeneza’ – Aminiel.
CRDT-MILLARDAYO

0 comments:

Post a Comment