.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
Wanaume ambao ni wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu.

Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.

Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi.

Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.

Waandishi wa waraka huo wa maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.

Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi.


Rod Stewart na mkewe Penny Lancaster
Wanafanya hayo, katika mazingira magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine na hata wanawake warefu wanaokutana nao.

Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa, lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha.

Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.

Nazo ni, wanaume wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti.

Hali ya kukata tamaa ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu hilo halliwajalishi.


Spika wa bunge la waakilishi Uingereza, John Bercow, na mkewe Sally

Moja wapo ya ufumbuzi wa ripoti hiyo pia ni kwamba wanaume wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume warefu, ingawa utafiti pia unaonyesha kwa wanaume wenye kimo kirefu, aina ya kazi zao za nyumbani inatofautiana.

Kwa maana nyengine, wanaume wafupi hawafiki juu ya makabati. Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa kwa sababu ya kutaka kuridhisha, bali wanadumu kwenye ndoa kwa sababu wanataka kuonekana.

Utafitio huu kama ulivyosoma hapo awali umeua mjadala mkali lakini pindi mtu anaposoma utafiti wao kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.

Hii ni licha ya mazingira magumu wanayokabiliwa nayo katika ndoa zao na hufanya hivyo na wake wafupi waliowaoa lakini pia na wanawake warefu wanaokuwa wamewaoa.

Utafiti huo unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana kasi ya kuoa lakini wanapooa wao hudumu katika ndoa zao.
Shukran kwa BBC

0 comments:

Post a Comment