.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
sitti_mtemvu_miss_tanzania_crown_taji
WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,  taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo. uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.
Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
FikraPevu imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18.

Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.
CRDT:williammalecelaBLOG

0 comments:

Post a Comment