.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
Groom placing a wedding ring on his Brides fingerKuwepo kwa mitandao ya kijamii kumeleta mambo mengi na mengine sio ya kawaida mfano tabia iliyopo siku hizi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakianzisha uhusiano mpaka wa kimapenzi kupitia mitandao hiyo na hawajawahi kukutana kabla, wapo wachache ambao wameweza kuvuka na kufikia hatua ya kuoana lakini wengi huishia barabarani.
“Wewe sio mwanamke niliyekuwa nakufikiria.. samahani, ila ninakuacha”  bwana harusi alisikika akisema hayo maneno siku ya ndoa baada ya kukutana uso kwa uso na bibi harusi siku ya ndoa yao huko Saudi Arabia.
Wageni waalikwa walishtuka na bibi harusi akapoteza fahamu huku ndugu na jamaa wakimsihi jamaa akubali ndoa hiyo iendelee, utamaduni wa nchi za mashariki ya kati, magharibi mwa Madina wapenzi huweza kuoana hata bila kufahamiana.
Bwana harusi huyu alimpa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga picha, maharusi hawa kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.
Medina
Medina
Unaambiwa Mwanamke huyuo alipofungua kitambaa alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu kwenye camera, mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla ambapo kwa mujibu wa gazeti la Okaz, mwanamume huyo alianguka na kuzirai.
Hata hivyo Bwana harusi aliliambia gazeti hilo kwamba hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi ambapo kauli zake ambazo haziwezi kusahaulika ni hizi >>> ”Si wewe msichana niliyetaka kuoa, si wewe kamwe niliyedhani kwa hivyo nakupa talaka’
Kingine kikubwa kilichoripotiwa ni kwamba baada ya Bibi Harusi kupewa talaka alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.
CREDT-MILLARDAYO

0 comments:

Post a Comment