Wiki chache Linah alianza kupost vipande vya picha na video ambayo wengi tulikua tukiona tu maandishi yanayosema inakuja,leo baada ya futari THT Linah ameitumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi video na audio ya wimbo huu.
Mtu wa kwanza kuinunua video hii ambaye ameingia kwa rekodi ni Cloud kutoka Bongo Movie ambaye alipoiona tu akatoa pesa akainunua,wapili ni Mrisho Mpoto ambaye nae hakutaka kusubiri zaidi.
Linah ameagwa rasmi na uongozi wa THT baada ya kupata uongozi mpya utakaoanza kumsimamia kazi zake ambazo kwa utangulizi wameanza na kazi hiyo iliyofanyika South Africa kuanzia audio hadi video na kampuni hiyo inaitwa No Fake Zone Entartainment.
.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
Posted by kifesi |
Msanii wa muziki kutoka Nigeria hit maker wa ‘Aye’, Davido ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Davido ametumia kiasi cha zaidi ya milioni 60 kununua saa ya dhahabu aina ya ‘Gold Rolex Sky-Dweller’.
Mkali huyo wa ‘Skelewu’ kupitia instagram ameandika: ‘Been working too hard lately so l decided to spoil myself’.
Add a comment
Subscribe to:
Posts (Atom)