Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL
ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni
pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na
Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha
mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:
Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story
zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile,
sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na
that situation..?“
Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki
ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie
hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio
mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa
mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni
kawaida…“
B 12 :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?…”
Diamond :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri…
Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni
kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana
ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “
B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“
Diamond :- “… Sijui…“
B 12 :- “…Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu
wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba
inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia
japokuwa bado kama kakutosa hivi…“
Diamond : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu
ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa
hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:
Diamond :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio
nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka
kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na
mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa mimi nikiwa Nigeria basi
Davido anipokee hivyo hivyo…“