Tuzo za watu zimefanyika usiku wa tarehe 27/6 kwenye hotel ya Serena Hotel.Baadhi ya tuzo zilienda kama hivi, Muigizaji wa kike anayependwa-Elizabeth Michael, Mwigizaji wa kiume anayependwa – Mzee Majuto,Video ya muziki ya muimbaji wa kiume imeenda kwa Diamond Platinumz (My number 1),Lady Jay Dee ameshinda tuzo ya video inayopendwa ya muimbaji wa kike na video ya Yahaya. Tuzo ya mtangazaji wa radio anayependwa ni Millard Ayo na show ya radio inayopendwa ni Amplifaya.
Filamu inayopendwa imeenda kwa Ndoa yangu, Juma Kaseja akishinda mwanamichezo anayependwa, Nisher ameshinda ya muongozaji wa video anayependwa,Salim Kikeke ameshinda ya mtangazaji wa TV anayependwa, Salama Jabil ameshinda ya mtangazaji wa TV wa kike anayependwa na nyingine ziliendelea.