Daily Mail imeripoti kuwa msichana huyo wa Colorado, Marekani amekutwa hana hatia na mahakama baada ya vipimo vya madaktari kuonesha kuwa ana matatizo ya akili na hata wakati anafanya tukio hilo hakuwa sawa kiakili.
Mahakama hiyo imeamua kuwa Isabela apelekwe hospitali kuanza matibabu badala ya kwenda jela kama ilivyokuwa inatarajiwa na wengi.
Upelelezi wa polisi ulieleza kuwa msichana huyo alimuua mama yake aitwae Yun Mi Hoy kwa kumchoma visu usoni mara 35, shingoni na sehemu ngingine za mwili wake.
Isabella anaelezwa alikuwa anamtishia mama yake mara kwa mara kuwa atamuua.
0 comments:
Post a Comment