.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Siku chache baada ya mke wa mjukuu wa Malkia Elizabeth , Kate Middleton kujifungua mtoto wake wa pili ambaye ni mtoto wa kike , hatimaye mtoto huyo amepewa jina baada ya siku kadhaa za watu nchini Uingereza kuwa katika hali ya kusubiri kwa hamu ili kuweza kufahamu jina la binti huyo .
Familia hiyo change imempa jina la Charlotte Elizabeth Diana ikiwa ni kuwaenzi bibi , bibi mkuu na babu mkuu wa mtoto huyo ambao walikuwa na majina aliyopewa .
Familia iliamua kuwa katika majina matatu ya mtoto huyo liwepo jina la mama yake Prince William ambaye ni Hayati Princess Diana ambaye ni bibi wa mtoto huyo , Bibi yake Prince William kwa upande wa baba yake ambaye ni Malkia Elizabeth na babu wa mtoto huyo mchanga ambaye ni Prince Charles ambaye ni baba mzazi wa Prince William kupitia jina la Charlotte ambalo ni jina la kike la Charles.
Jina rasmi la mtoto huyo ambaye alizaliwa siku tatu zilizopita litakuwa’Her Royal Highness Princess Charlotte Elizabeth Diana Of Cambridge’.
Taarifa toka ndani ya familia ya kifalme Uingereza zinasema kuwa Prince William na Mkewe Princess Kate Middleton tayari walikuwa wameandaa jina hilo saa chache baada ya kuzaliwa kwake na walingoja wakati muafaka kutoa taarifa kwa ndugu wengine wa familia .
Mtoto huyo alikutana na Malkia Elizabeth kwa mara ya kwanza hii leo wakati familia yake ilipokwenda kusalimiana na Malkia huyo nyumbani kwake kwenye Kasri la Buckingham.
Princess Charlotte Elizabeth Diana anakuwa mtoto wa pili wa familia ya Prince William baada ya George Alexander ambaye alizaliwa miezi 21 iliyopita .
Subscribe to:
Posts (Atom)