Huffington Post limeripoti habari kutoka Uingereza ya
kusikitisha ya kijana Rhys Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake
Chanttelle Ward mwenye umri wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na
ugomvi unaohusisha na wivu wa mapenzi.
Kijana huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa
mpenzi wake alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook akimsaliti.
Akisimulia mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza
kuwa baada ya kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake
msichana huyo walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo
akimtuhumu kuwa anamsaliti kupitia Facebook.
Kijana huyo alichukua simu ya Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia
jumbe alizokuwa anatuma Facebook lakini hakukuta mawasiliano kati ya
msichana huyo na mwanaume aliyekuwa anamhisi. Moja kwa moja akaanza
kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa amezifuta.
Hasira za kijana huyo zilimuogopesha akaona ni bora ampigie simu mama
yake lakini alinyang’anywa simu. Rhys alifunga mlango na kuendelea
kumshambulia kwa maneno.
Chanttelle anaeleza kuwa mgogoro huo ulipofikia hatua ya kupoa hivi,
kijana huyo alimkiss huku akimuuliza kama kweli ana mpenda na hapo ndipo
kila kitu kilibadilika.
“Aliweka mdomo wake wote kuzungumguka lips zangu na kuvuta, nilidhani
lips zote zimetoka. Damu zilisambaa kila sehemu.” Msichana huyo
alieleza.
Polisi walipofika walikuta wote wametapakaa damu usoni, wakamkamata
kijana huyo na kumkimbiza Chanttelle hospitali huku akiwa na mikwaruzo
katika sehemu mbalimbali za mwili.
Mwanaume huyo alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo, alieleza
kuwa hakuwa na nia mbaya ya kumuumiza mrembo wake ambaye anadai alikuwa
na bahati kuwa naye.
Rhys alikutwa na hatia. Alirudishwa rumande na anasubiri hukumu yake mwezi ujao.