.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
 KEYSHIACOLE_PONR
Siku chache baada ya kukamatwa na polisi kwa kumpiga mwanamke aliyekuwa na mpenzi wake ambaye ni Birdman, Keyshia Cole ametangaza nyimbo na cover la album yake mpya ya  “Point Of No Return” . Wasanii walioshirikishwa kwenye album hii ni pamoja na 2 Chainz,Future, Wale, August Alsina na Juicy J.
 1. “Intro (Last Tango)”
2. “Heat of Passion”
3. “N. L. U” (feat. 2 Chainz)
4. “Next Time” (Won’t Give My Heart Away)
5. “Rick James” (feat. Juicy J)
6. “Do That For (B.A.B.)”
7. “New Nu”
8. “She”
9. “Believer”
10. “On Demand” (feat. Wale & August Alsina)
11. “Love Letter” (feat. Future)
12 “Party Ain’t a Party” (feat. Gavyn Rhone)
13. “Remember (Part 2)”


Posted by kifesi |
Siku mbili baada ya Amber Rose kufuata taratibu za kisheria akidai talaka kwa mumewe Wiz Khalifa, Nick Cannon ameendelea kunyoshewa vidole kuwa chanzo cha yote na kudaiwa kuchepuka na mrembo huyo kwa kipindi kirefu.
Chanzo kimeiambia TMZ kuwa Nick ambaye hivi sasa ni meneja wa Amber Rose amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa hajawahi kuchepuka na Amber na hahusiki kivyovyote na uamuzi wake.
Ameeleza kuwa alikuja kufahamu Amber Rose alikuwa na matatizo ya kifamili kupitia mwanasheria wake wiki iliyopita. Nick anasema baada ya kufahamu hivyo wawili hao walianza kushare masimulizi ya kuacha na kuachana.
Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Wiz na Amber Rose, kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa michepuko.

Amber Rose, Wiz Khalifa na mtoto wao
Tangu taarifa hizo zilipoanza kusambaa, Amber Rose amekuwa akipost picha na jumbe za ajabu kwenye Instagram na Twitter akionesha mwili wake.
Kwa upande wa Wiz Khalifa amekuwa akitweet jumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na “Everyone deserves to be loved”.
Hayo yanajiri wakati ambapo Nick Cannon yuko kwenye wakati mgumu akisubiri uamuzi wa mkewe Mariah Carey kudai talaka kisheria au kurudisha ndoa yao ambayo hivi sasa iko vipande.
Posted by kifesi |

 Exclusive: Babu Tale azungumzia ujio mpya wa Diamond, kazi zote zimetayarishwa nje
Wakati wimbo wa MdogoMdogo ukiwa bado unasumbua kwenye media, Diamond Platinumz anatarajia kurusha mawe mengine mazito zaidi kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wake.
Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond amesema mkali huyo anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo na kwamba zote zimetayarishwa nje.
“Tusubirie kidogo, baada ya miezi miwili mitatu tutaongea kwa sababu kuna kazi zinakuja, Diamond anarelease ngoma mbili mfululizo na zote zimetoka nje. Lakini hatuwezi kueongea sasa hivi hadi muda ufike.” Babu Tale ameiambia tovuti ya Times Fm.
Exclusive: Babu Tale azungumzia ujio mpya wa Diamond, kazi zote zimetayarishwa nje
Posted by kifesi |











Posted by kifesi |
Mashabiki wa shindano la Big Brother Africa wanaoisubiria kwa hamu msimu mpya utakaoanza mwezi ujao uliopewa jina la ‘Hot Shots’.
Hivi karibuni wametajwa washiriki wengine sita wanaoziwakilisha nchi zao. Kutoka Tanzania mrembo Irene Laveda ambaye ana kipaji cha kuigiza anaungana na Idris ambaye ni mpiga picha  kuiwakilisha nchi yetu katika jengo hilo.
Angalia picha za washiriki hao sita waliotajwa hivi karibuni.

Laveda (Tanzania)

M'am Bea (Ghana)

Luis (Namibia)

Lilian (Nigeria)

Kacee Moore (Ghana)

JJ (Zimbabwe)
Posted by kifesi |
 http://ionetheurbandaily.files.wordpress.com/2012/03/wiz-khalifa-amber-rose-2011-getty-c-flanigan-cropped.jpg
Tmz wameripoti kuwa model Amber Rose ameomba talaka kutoka kwa mume wake ambaye wameishi pamoja kwa muda  wa mwaka moja. Amber anasema yeye na mumewe wametengana kuanzia Jumatatu na anataka haki zote za malezi za mtoto wao Sebastian mwenye umri wa mwaka mmoja.
Tofauti na ndoa za wasanii wengine zikivunjika hugawana pesa na mali, Amber alisainishwa makubaliano ya kutochukua mgao wa pesa au mali kutoka kwa mumewake endapo watatengana.