
Kuwafanyia Ihsani Wazazi Allah sub-hanahu wa ta’ala amesema:
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na
wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako,
au wote wawili, basi usimwambie hata uff (yaani ah kwa wazungumzaji wa
Kiswahili) Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. (17: Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo...