Nimeleta hii kitu hapa ili mjifunze, hii mitandao sasa inavunja sana ndoa. Hadi michepuko wapi wanatafuta online ni hatari. Hivi watu wa jinsi hii hawaogopi ukimwi? Hawana hofu ya Mungu? Kwa nini unadanganya kwa watu upo single na wakati una mke na mtoto. Sasa haya ndio matokeo yake.
Huyu ni mume, kama hayupo kazini akiwa nyumbani muda wote yupo kwenye internet. Imefikia hatua anaweza kesha kwenye computer au simu. Ukiiuliza nini haswa unatafuta online, anasema naangalia news za nyumbani Tz. Yeye na mkewe wapo abroad. Kumbe ana mambo anayafanya nyuma ya computer. Huwezi amini ni mume na wana mtoto mmoja na mkewe ila vitu anavyofanya ni vya ajabu.
Mkewe katika kuchunguza kagundua mumewe anachat na wanawake huko Tanzania, na mbaya zaidi mume trips za kwenda Tz haziishi, kumbe anafuata mabinti. Mke kafuma messages nyingi akiwasifia mabinti tofauti tofauti na mabinti waanatuma hadi picha wakiwa naked kwa huyo mume.
Mke alivyogundua, akaona isiwe shida ya kuleteana magonjwa na mkewe ndio kwanza yupo miaka 30.
Mwanamke kaamua kudai talaka huko huko abroad, ila mume anagoma. Unajua mambo ya nje hakuna longo longo kama Tz. Mwanamke kaenda kwa mwanasheria na kufile talaka. Mume sasa ana haha, maana ughaibuni hakunaga mambo ya kuhonga kama Tz.