Jamaa
alijipanga mwenyewe ili aachane na maisha ya ukapela, ndugu jamaa,
marafiki wakakutana ukumbini kwa ajili ya kusherehekea ndoa yake..
kilichotokea kiliifanya siku hiyo kuwa katika historia ya matukio ambayo
sio mazuri kwake.
Bwana harusi huyo Kang Hu wa China aliwashangaza wageni waalikwa kwenye harusi yake baada ya kukutana na bibi harusi, Na Sung kwa mara
ya kwanza siku ya harusi yao, lakini hakuvutiwa na sura yake na kuamua
kutamka kwamba hajavutiwa na muonekano wa bibi harusi huyo.
Sherehe hiyo ilivurugika, jamaa akatoka
kwa aibu, akatoka nje kwa hasira na kwenda kujitupa kwenye mto uliokuwa
karibu na ukumbi huo katika mji wa Shiyan, watu waliokuwa wakipita
karibu na mto huo walimuona na kutoa taarifa Polisi ambao walifika na
kumuokoa.
Pal Chan Wang aliyekuwa kwenye sherehe hiyo amesema familia ya Kang ndiyo
ilikuwa imemchagulia mwanamke huyo na kumlazimisha kumuoa lakini hakuwa
chaguo lake wala hakuwahi kumuona kabla ya siku ya ndoa, hii sio mara
ya kwanza kutokea tukio la harusi kuvunjika siku ya ndoa.
CRDT;MILLARDAYO.COM
0 comments:
Post a Comment