Alhamis ya jana (November 14) mwanaume mrefu kuliko wote duniani na
mfupi kuliko wote walikutana katika tukio lililofanyika London ambapo
walipiga picha ya pamoja wakipeana mikono.
Tukio hilo
lilikuwa ni lakumi la mwaka la rekodi za Guinness kusherehekea rekodi
zilizowekwa na dunia. Guiness waliwasafirisha wanaume hao ambao ni
Sultan Kosen kutoka uturuki (Mrefu) na Chandra Bahadur Dangi (mfupi)
kutoka Nepal kwaajili ya picha ya kipekee.
Kosen
(31) ni mkulima wa msimu mwenye urefu wa feet 8na nchi 3, ana uwezo wa
kushika kikapu cha goli la bascket bila kuruka, alishika rekodi hiyo
mwaka 2009 baada ya kumpita urefu Xi Shun wa China mwenye feet 7 na nchi
9
Dangi (74) yeye ana urefu wa nchi 21½ na ni mwanaume mfupi aliwahi ku-rekodiwa na Guiness na ana uzito wa Pound 32