.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Katika
kitu ambacho hakikutegemewa kabisa kutokea licha ya yeye mwenyewe
kuweka ahadi, ni Roma kuingia ndani ya Sharobaro Records na kufanya kazi
na producer Bob Junior. Lakini amini usiamini Roma amekamilisha ahadi
yake na ameingia Sharobaro Records na ku record na Bob Jr.
Wiki
mbili zilizopita wakati mchezo wa fainali za kombe la dunia
zikiendelea, wakati Brazil na Argentina zikiwa uwanjani, Msanii wa
Hiphop ambae kazi zake nyingi hufanyika Tongwe Records Roma, alipost
picha yenye maneno yanayosema
matokeo
yake Brazil wakachapwa tena goli 7 kwa 1, kwa kipigo kile kitakatifu
Roma hakutaka kuzungumzia ishu hiyo hata baada ya kupigiwa simu.
Lakini jana Roma alipost picha akiwa na Bob Jr ndana ya studio za Sharobaro na kuandika
Real
NINJA always lay...on his words!! Xo am xtand on ma' words!!!! Last nyt
baada ya ftari tu...nikapiga ndefu hadi TONGWE nikagonga ngoma moja na
#josmtambo# Kisha nikamchukua producer wangu wa TONGWE REC...tukaenda
wote kwa BOB JUNIOR!! SHAROBARO REC!! Wakakaa kiti kimoja.... Bob
junior(sharobaro rec)+ geof master(tongwe rec)!!!===== Wakagonga BEAT!!!
Guess what.......!!! We makin history!!
Kwa upande wake bob jr yeye amesema
ilikuwa poa kabisa kwasababu kaja moja kwa moja nimemsikilizisha beat alikuja na idea yake kabla sijamsikilisha beat, lakini nilipomsikilizisha beat idea yake akaiweka pembeni kakubali sana nilichokifanya, wimbo unaitwa maumivu, ni bonge moja la ngoma. hii ngoma mi nimeimba chorus ye anachana halafu kwenye verce tunajibishana ye akichana mi naimba kwahiyo mungu akijaalia wiki ijayo itatoka....endelea kumsikiliza hapo chini
Posted by kifesi |
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo mwaka 2011.
Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa gerezani pamoja na mume wake ambae ni raia wa Marekani mwenye asili ya Sudan, waliwasili Italy wakiwa wameongozana na Afisa wa Italia ambae alisaidia kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan ambayo iliwashikilia Meriam na mumewe kwa wiki kadhaa baada ya kuwakamata Airport wakiondoka nchini humo.
Video iliyotolewa na Vatican imemuonyesha Pope akimpa Meriam medali pamoja na rozari ambapo baada ya kukutana na Pope, wawili hawa wakiwa na watoto wao watambatana kuelekea nchini Marekani ambako ndiko makazi yao yalipo New Hampshire alikowahi kuishi mume wa Meriam.
Afisa wa Italia aliehusika kuongea na serikali ya Sudan ili familia hii iachiwe, amesema ilibidi wawe wapole kwenye maongezi na ndicho kilichosaidia mwishoni wakaachiwa huru baada ya kushikiliwa pamoja na kwamba Mahakama kuu ya Sudan ilimuachia huru Meriam.
Meriam mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
Meriam mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
Subscribe to:
Posts (Atom)