Amber Rose aliwashtua mashabiki wake na Wiz Khalifa baada ya kuripotiwa kutengana na mumewe huyo huku akifanya taratibu za kupata talaka yake kisheria.
Baada ya taarifa hizo kusambaa kwenye vyombo vya habari siku mbili zilizopita, iliripotiwa kuwa chanzo cha yote ni Amber Rose kuchepuka na mme wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye pia ndoa yake iko katika sintofahamu.
Hata hivyo, Amber Rose amethibitisha kuwa Wiz Khalifa alikuwa akimsaliti na wanawake wengine huku akikanusha vikali tuhuma za kuchepuka na mwanaume yeyote kwa kipindi chote cha ndoa yao.
Ameendelea kusisitiza kuwa hivi sasa anakijikita katika malezi ya mtoto wao wa kiume, Sebastian.
Amber ameandika tweet kadhaa kupitia twitter kuhusu sakata hilo.
.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Subscribe to:
Posts (Atom)