Mwaka
2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani wa
Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu
lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona
wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi,
huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja
limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga?
Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa
habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae
aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu
kudanganya umri, elimu na mambo mengine.
Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja
akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto
na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna
uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ –
Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas
Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana
kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na
wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa
hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao
ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli
ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja
kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo
huo’ -
Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya
kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na
lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza
pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli
walishawishika na ndio maana akashinda’ –
Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana,
katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya
kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa
May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga
‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti
vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia
hivyo vyeti vyao Original’ –
Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache
zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa
akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi
sio ya kwetu’ –
Lundenga
Baada
ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache
kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa
kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -
Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti
Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya
maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji
kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ –
Sitti
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>>
‘Nadhani
inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka
tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu
ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari
vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka
1989,
Sitti amesema ‘Sitogusia hilo
swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha
kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na
nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya
kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’