.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |


MISS TZ 3Mwaka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani  wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga?
Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.
Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’ - Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga

‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga
Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’

0 comments:

Post a Comment