.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe
kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G
Habash imevunjika.
Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha
Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye
uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya
kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa
akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa
siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi
kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu
ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye
media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote
ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha
yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote
wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu
anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee
kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na
privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza
kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au
mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote
anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za
watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja
wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili.
“Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil
Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Credit Bongo5
Posted by kifesi |
Picha
hizi zilisambaa miezi michache nyuma ambazo zilikua zikimuonyesha Ommy
Dimpoz kama katoka kijijini amekuja mjini,zilizua maswali mengi sana na
baadae alisema zilivuja maana zilikua zikihusu tamasha la Serengeti
Fiesta.
Video yake imeongozwa na Adam Juma kutoka Next Level,ndani ya video hii yupo
Video yake imeongozwa na Adam Juma kutoka Next Level,ndani ya video hii yupo
pia
mrembo Jokate ‘Jojo’ ambaye wanaonekana kwenye treni wakisafiri,hii ni
remix iliyopigwa ki midundo ya mchiriku zaidi baada ya ile ya
kwanza,humu kashirikishwa Msaga Sumu.
Subscribe to:
Posts (Atom)