Mwanamuziki maarufu wa nchini Uganda, Juliana Kanyomozi, leo asubuhi
amempoteza mtoto wake mdogo wa kiume Keron baada ya kusumbuliwa na
ugonjwa wa Pumu. Kwa mujibu wa gazeti na New Vision Keron amefariki
katika hospitali ya Aghakhan.

Ni wakati mgumu kwa mwanamuziki huyo mrembo kwakuwa amekuwa akimpenda sana mtoto wake wakati akithibitisha taarifa hizo.
New Vision imemnukuu Juliana akisema kuwa” Malaika wangu ametangulia
kwa Mungu, kilichosambazwa awali ni uzushi. Amefariki leo saa 10:25
asubuhi hii, amekuwa mpambanaji mkubwa wa afya yake nawashukuru wote kwa
maombi yenu nitajitahidi kujikaza, Mungu amlaze mahali pema Keron lala
salama mwanangu hadi tutakapokutana tena.”
Juliana amewaomba mashabiki wake kumuombea mtoto wake huyo haswa katika kipindi hiki kigumu kwake.
Juliana amesema mtoto wake hakuwa katika hali nzuri baada ya kushambuliwa na ugonjwa wa Pumu uliomsababishia kupoteza maisha.
crdt-millardayo