Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la
Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi
kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha
njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.
Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia
kuhama kutoka kwenye makazi
yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema
watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam
amesisitiza hali sio nzuri hivyo
wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata
wanaotembea na magari barabarani kwa sababu
njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo
lazima barabarani.
Hizi ni baadhi ya picha kati ya
nyingi zinazosambaa kwenye mtandao.
0 comments:
Post a Comment