Hizi ni taarifa zingine za ghafla ambazo Tanzania
tumezipokea kwa mshtuko na masikitiko ni kifo
cha miongoni mwa-madirector wa Tanzania ambao
ni waigizaji pia,huyu ni Adam Kuambiana ambaye taarifa
za kifo chake zimeanza kusambaa mchana wa
Mei 17.Mwenyekiti wa Bongo Movie
Steve Nyerere amesema>>’Mwenzetu Adam Philipo
Kuambiana amefariki akiwa Location ana shoot
,mimi nimepigiwa simu saa 3 asubuhi kuwa hospitali pale
Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli Adam
amefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam
Kuambiana amefariki’
‘Sasa hivi tumetoka Muhumbili
kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema
wakati yupo location alikua analalamika tumbo linamuuma
linamuuma kumfikisha hospitali ndipo umauti ukamfika’
.
Kwa mujibu wa Steve Nyerere amesema kuwa marehemu
Adam kuambiana alikua ana shoot filamu yak
e mpya ambayo ndani yake amewashirikisha
wasanii kadhaa wa Bongo fleva akiwemo Q Chillah
0 comments:
Post a Comment