Mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa
kesi za mauaji wameleta kizaazaa baada ya kujaribu
kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa na
kuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.
Tukio hilo
limetokea May 7 2014 saa nne asubuhi katika
Mahakama ya Hakimu
Mfawidhi wa Wilaya ya
Nyamagana Mwanza walipofikishwa kwa ajili ya
kusikilizwa kwa kesi zao lakini ghafla walipofika kwenye
viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbio
kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya
Taifa na kuvua nguo kisha kuanza kupiga
kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.
Ni Thobiasi Warioba (35) alieamua kuvua nguo zote na
kubaki mtupu eneo la mlingoti wa bendera ya taifa,
ambaye anakabiliwa na kesi ya
mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa wengine
waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35),
Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine
ambaye hakufahamika majina
yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013 na
walikamatwa tangu mwaka 2011.
13
Baada ya kudhibitiwa na askari polisi walisikika wakisema:
“haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi
sasa kesi zetu hazijasikilizwa, wengine tumebambikiziwa
kesi tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya
habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila
kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011
tulipokamatwa, tumechoka kukaa mahabusu
tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada ya malalamiko
yao askari mmoja aitwae Inspekta Henry akiwa n
a wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie
aliwahoji kuhusiana na madai yao huku askari hao wakiwataka
kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka
Warioba avae nguo ili waweze kuingia Mahakamani.
Warioba avae nguo ili waweze kuingia Mahakamani.
15Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Mwanza ambae alikataa kutajwa
jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao
bado haujakamilika na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa
na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake
zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.
17
16
SONY DSC
18Unataka stori kama hizi zisikupite? jiunge
na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo
la @millardayo na nitakua nakutumia stori kama hizi kila zinaponifikia.
0 comments:
Post a Comment