.

.

NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA

Gallery

Posted by kifesi |
 
Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta mamia ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo,baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Gea Habib wa Hekaheka ameongea na mashuhuda wa eneo hilo ambalo wameshuhudia viungo hivyo kabla ya kuchukuliwa na jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.

0 comments:

Post a Comment