.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Guy Scott ambaye alikuwa makamu wa rais
Zambia wakati wa utawala wa Michael Sata ametajwa kushika nafasi ya
urais wa nchi hiyo kwa sasa mpaka pale ambapo ataapishwa mara baada ya
kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Waziri wa ulinzi Zambia Edgar Lungu
amesema maandalizi ya uchaguzi huo yataanza muda wowote ambapo katiba ya
nchi hiyo inaagiza kufanyika uchaguzi wa Rais ndani ya siku 90 baada ya
kufariki kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.
Scott ameteuliwa kushika wadhifa huo
ambapo hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais mzungu kuongoza nchi ya
Afrika tangu kuisha kwa kipindi cha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini chini
ya utawala wa FW de Klerk.
Posted by kifesi |
Wiki moja baada ya kutokea kwa msiba wa mmoja wa wasanii wa TMK Wanaume Family YP na saa chache baadaye ukatokea msiba mwingine wa aliyekuwa msanii wa maigizo na vichekesho Sherry Mwana, leo Oktoba 30 umetokea msiba mwingine Bongo Movie.
Taarifa za awali zimeanza kusambaa
kupitia watu mbalimbali maarufu Tanzania ambao wameaanza kuonyesha
masikito yao akiwemo msanii Bob Junior kuhusu kifo cha mzee Manento
ambaye inadaiwa amefariki jana usiku.
CRDT:millardayo.com
Posted by kifesi |
Taarifa ambazo zimetoka muda mfupi uliopita zinasema kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ asubuhi ya leo October 29 amepata dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa.
Chid Benz alipandishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana October 28 na kusomewa mashtaka matatu yaliyokuwa yakimkabili ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Leo asubuhi amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya,kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tena October 11 mwaka huu 2014.
Source:Globalpublishers.com
Subscribe to:
Posts (Atom)