sehem ya kisiwa cha hawaii |
Ukiwa na pesa hapa duniani bila shaka hakuna
utakaloshindwa kulifnya kulingana tu na ulefu wa pesa yako,sikia
hii,,Mmiliki wa mtandao mkubwa wa kijamii Facebook
Mark Zuckerberg amenunua
sehemu kubwa ya kisiwa cha Hawaii iitwayo Kauai kwa
dola za Kimarekani milioni 100 jarida la Forbes limeripoti.
Eneo hilolitajumuisha beach resort, mashamba ya miwa na
kilimo
hai ambapo kwa sheria za Hawaii beach resort hiyo
lazima iachwe wazi
kwa matumizi ya jamii kwa
sababu kisiwa hiko hakina sheria ya umiliki
binafsi wa mchanga.
Zuckerberg anakua ni bilionea wa pili kununua sehemu ya
Hawaii.
Mwaka jana mwenyekiti wa Oracle
Larry Ellison alinunua upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa dola milioni 600
0 comments:
Post a Comment