MWANAMITINDO maarufu
nchini, Hamisa Mabeto
ametishia maslahi ya wasanii wa
kike wa Bongo Movie
baada ya kujitosa rasmi kwenye tasnia hiyo na
kung’ara katika Filamu ya
VIP akiwa na mastaa, Vincent Kigosi ‘Ray’ na
Jacqueline Wolper.
“Wasanii w
ajiangalie nafasi zao baada
ya Mabeto kuingia kwenye filamu maana ndani ya
VIP amekamua sana na wasipokuwa makini atawasumbua
kutokana na mvuto ulionao,” alisema Ray.
Mabeto ametamba kwenye ulimbwende tangu mwaka 2010
alipoibuka mshindi wa shindano XXL Back to School
Bash.
Mwaka 2011 alishika nafasi ya
pili katika shindano kumsaka Miss Dar Indian Ocean
na baadaye Miss Kinondoni.
Mwaka 2011 alishiriki
Miss Tanzania na kufika hatua ya nusu fainali ya michuano
hiyo. Mwaka 2012 akafika hatua ya kumi bora kwenye Miss University.
0 comments:
Post a Comment