Katika hali ya Kuonesha Mshikamano na
Umoja wa Watanzania hususani hapa Marekani
tar 27/04/2014 Watanzania walikutana tena
Kwenye Tamasha la Michezo na Nyama Choma
kwa Lengo la Kuimarisha Umoja na Muungano wetu
uliochini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tamasha limefana sana na Watanzania wamejitokeza
kwa WIngi Kutoka Majimbo mbalimbali hapa
Marekani wamefika Washington Kujumuika pamoja
,Ni tukio la aina yake ambalo Watanzania na Familia
zao wameweza Kujamiiana na
Kufahamiana Vizuri mbali na Maisha yao ya Kila siku hapa Marekani.
Katika Mchezo wa Mpira wa Miguu,Mchezo umemalizika
kwa sare ya Magoli 2 kwa 2 ambapo Kilimanjaro
Stars walifanikiwa Kupata Magoli yote mawili
kipindi cha Kwanza na Baada ya Mapumziko
Zanzibar Heroes wakafanikiwa
Kurudisha Magoli yote Mawili hali ilioleta msisimko
Mkubwa sana kwa Mashabiki hasa Ukizingatia Kipindi
hiki Watanzania wanapigania Serikali mbili
ziendelee Kuwa nguzo za Muungano wa
Tanzania,Hivyo Magoli Mawili
kwa kila Upande
wa Muungano yaweza Kutafsiriwa kuwa ni Kuunga
Mfumo wa Serikali mbili(Ni Mawazo Binafsi)
Mwisho wa Mchezo timu zote Mbili zilifanya Maridhiano
ya Kila timu Iinue Kombe na Kushangilia na
baadae Kumkabishi Balozi Libereta Mulamula.
Picha/Maelezo na Festo Sanga-Washington DC.
Mh.Nchemba akiongozana na
balozi Mula mula kwenda kufungua tamasha
Nyama na sausage zikichomwa
Mambo ya u-canon na mmoja wa rafiki
Mh.Nchemba akikagua Team zote kabla ya mchezo
Mchezo ukawa hivi
Mashabiki wa Kilimanjaro stars
hatukuwa na tatizo na mtuu
0 comments:
Post a Comment