Orodha ya wasanii watakaoshiriki kwenye
Kili Music Tour 2014 imetangazwa leo. Baadhi ya
wasanii watakaokuwepo kwenye ziara hiyo
wakiwe kwenye picha ya pamoja Mwaka huu
zaidi ya wasanii 30 watashiriki katika
ziara hiyo kwenye
mikoa zaidi ya 10 nchini na itakayoanza ambao Mei
hadi Septemba 2014. Wasanii hao
ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex,
Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala
Jeremiah,
Fid Q, Snura, Weusi,
Ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole na Mwasiti. Wengine ni
Nay wa Mitego, Mwana FA,
Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the
East, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Vanessa
Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian Bella
.
Hata hivyo Lady Jaydee
aliyekuwepo kwenye ziara hiyo mwaka jana,
ameondolewa mwaka huu kwa kile chanzo kimoja
kimesema ni kutokana na tweet ya dharau aliyoiandika
Lady Jaydee kuhusu kutokufahamu kama tuzo hizo
zilifanyika.
Chanzo hicho kimesema pia kuwa Roma
alikuwa awepo kwenye ziara hiyo lakini ‘ujuaje
wake
umemfanya apigwe chini’.
0 comments:
Post a Comment