Kwenye Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa
The Sporah show, Jaq amekanusha kwamba yeye ni
msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa kiume
na kusisitiza ‘sasa hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za
kiume, wengi walikua wanahisi lakini sijawahi kufanya
vitendo vya usagaji na wala sijawahi kushawishiwa na mtu
anaejihusisha na vitendo hivyo, boyfriend wangu
hana tatizo na mavazi ya kiume ninayovaa…
hatujawahi kupangiana mavazi’
Kwenye jibu jingine
alilotoa J\ anasema ‘sijaolewa na wala sijawahi kuolewa,
nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na
usimuhukumu mtu bila kumuuliza’
Sporah: Ni kweli kwamba
ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu
unataka akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka
ubadilishe dini ili upate hizo mali?
J Wolper:
‘Sio hivyo, dini nilikuja kubadilisha wakati
nimeshapata mali, nilibadilisha mwishoni kabisa baada ya
huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa, alinipa
mali na vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana
, unajua unaweza ukawa unachat na mtu mkapendana
lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi,
unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze
kukushawishi mkapendana wakati yeye yuko mbali na wewe
uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo wala
sura bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri
mpaka nikaona huyu ni sahihi nikabadilisha dini’
Screen
AMSporah: Ulifikiri
a kwamba dini yako sio nzuri au?
J Wolper:
‘Kwa utamaduni wetu sisi Afrika, Tanzania
ninavyojua hata kwa mama yangu imetokea,
Mwanamke lazima ufate dini ya Mwanaume wako
’
Sporah: Lakini alikua bado hajakuoa?
J Wolper: Nilikua tayari nimeshajiona kama mke wake
, ni mtu ambae alinipenda sana…
Sporah: Ulijichora na tatoo
ya jina lake?
J Wolper: Kwa nini nichore jina la mtu
kwenye mwili wangu, kwanza yeye ni Muislamu
hapendi tatoo… nilibadili dini kwa mapenzi yangu
mwenyewe kutokana na mtu niliekua nae na hawajui
alivyonishawishi mpaka mimi nikabadili, sio kwa kulazimishwa…
.
‘Ninachojua mimi heshima ni kufata dini ya Mwanaume
ukishachumbiwa, haikua kama girlfriend na boyfriend…
alikua ananifanya kama mke wake japo hatukua
tumekutana’ – J Wolper
Sporah: Ulijisikiaje pale
vitu havikwenda vizuri?
J Wolper: ‘Mi naona ni sawa tu
kwa sababu Mungu pia anapanga ila sikuumia sana,
ningeumia kama mimi ndio ningekua nimetaka kuolewa
ila yeye ndio alitaka ndoa, mimi bado mdogo… watu wa
mitandao kwao ni big deal ila kwangu sio kitu’
\\Haukuwa uamuzi mgumu, napenda sana kufata
moyo wangu… siwezi kufata moyo wa mtu, wengi
waliniambia sijui ukibadili dini tena sijui mashabiki wako
sijui nini nini… NOOOO! sio kuhusu mashabiki, mimi ni
mimi kama mimi sikupenda kilichotokea na bado niko
chini ya wazazi wangu, vp ikitokea nimekufa nitazikwaje
sijaolewa??! mi siwezi kumchezea Mungu ndio maana ukiangalia
instagram yangu mimi kila Jumapili lazima
niende kanisani’ – Wolper
J Wolper: ‘Nilikaa miezi miwili bila
kwenda Msikitini wala Kanisani, nilikonda kwa sababu
siwezi kukaa bila kusali na wazazi wangu nakua
nawakosea, kuna neno mama yangu mdogo aliniambia
baada ya kukaa na mama na kuongea nikasema ngoja
nirudi kanisani, siwezi kufaidisha watu na kuacha wazazi
wangu wakasononeka… nilibadili dini kwa heshima y
a mchumba wangu lakini sasa hivi nimerudi kwa heshima ya
wazazi wangu’
J Wolper: ‘Bado Dallas ni rafiki yangu
mkubwa sana kwangu na ni mtu poa, haongei mapenzi
maskini… ni rafiki yangu ni
kaka yangu, hatuwezi ten
a kuwa wapenzi… nampenda bado’
Unataka stori kama
hizi zisikupite? ungana na mimi twitter kwa kubonyeza HAPA
na nitakua nakutumia iwe usiku au mchana, pia facebook na instagram.
0 comments:
Post a Comment