Leo ningependa niweke uthibitisho wa dhidi ya madai
na maoni ya baadhi ya watu
waliopinga tangazo la
kwamba sijaalikwa kwenye
maonyesho ya tamaduni
yanayofanywa na Balozi
mbalimbali Washington, DC
na kubeba jina la PASSPORT
DC
yakiwa chini ya Caltural
Tourism DC na
yanayoadhimishwa
kila
mwaka wakati huu wa majira
ya spring.wanaodai
sijaalikwa sio kweli kwani muasisi
wa PASSPORT DC
alinifuata
baada ya kuona meza yangu
siku ya
\ maadhimisho ya
sherehe ya miaka 50 ya
Muungano
na kuniomba
barua pepe yangu na
kwamba angependa niwe
mmoja ya washiriki kwa
kuiwakilisha Tanzania na
pia
kama naweza kuonyesha
mitindo ya mbalimbali
ya
nguo za KWETU Fashions.
Baada ya
Hapo mawasiliano
yalianza na mimi kuweka
tangazo
langu kwenye
mitandao na waosha
vinywa kuanza
kusukutua
bila mswaki huku wengi
wakidai nadanganya na
wengine kulazimisha kuleta
vitu vyao bila kujua meza
zimetolewa kwa hesabu.
Mimi Barua yangu ya
mwaliko hii hapa mchana
kweupe na naomba
aliyejileta kwa kudai
maonesho
yalikuwa ya wazi
naomba nae alete barua
yake ya mwaliko
hapa ama kwenye blog ya Vijimambo.
hii ndiyo barua ya mwaliko
0 comments:
Post a Comment