Mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Marekani Angela Basset anatarajia kuongoza filamu itayohusu maisha halisi ya aliyekuwa mwanamuziki nguli duniani Witney Houston. Kituo cha Televisheni cha Lifetime cha Marekani kimethibitisha kuwa filamu hiyo itaelezea maisha ya Witney hadi kuibukia kwenye umaarufu pamoja na mahusiano yake na aliyekuwa mume wake kwa kipindi hicho Bobby Brown kuanzia mara ya kwanza walipokutana hadi kufunga ndoa. Mwanamuziki Witney Houston alifariki dunia February mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 48. Witney alikutwa amekufa chumbani kwake katika hoteli jijini Los Angeles. Angela Basset amecheza filamu nyingi zinazohusu maisha halisi ya watu ambapo pia aliwahi kucheza filamu ya hayati Notorious BIG akiwa kama mama yake na kutumia jina la Voletta Wallace.
.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Marekani Angela Basset anatarajia kuongoza filamu itayohusu maisha halisi ya aliyekuwa mwanamuziki nguli duniani Witney Houston. Kituo cha Televisheni cha Lifetime cha Marekani kimethibitisha kuwa filamu hiyo itaelezea maisha ya Witney hadi kuibukia kwenye umaarufu pamoja na mahusiano yake na aliyekuwa mume wake kwa kipindi hicho Bobby Brown kuanzia mara ya kwanza walipokutana hadi kufunga ndoa. Mwanamuziki Witney Houston alifariki dunia February mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 48. Witney alikutwa amekufa chumbani kwake katika hoteli jijini Los Angeles. Angela Basset amecheza filamu nyingi zinazohusu maisha halisi ya watu ambapo pia aliwahi kucheza filamu ya hayati Notorious BIG akiwa kama mama yake na kutumia jina la Voletta Wallace.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment