Mh.Rais Kikwete ametokea kutaja tena jina la Diamond Platnumz, akiongelea mengi waliofanya kipindi walipokutana na mkali huo wa AfroPop, Diamond Platnumz, akiwa anafunguka wakati alipokuwa anaongea na wasanii kule jijini Dodoma, jambo la kushangaza zaidi ambalo kila mtu hakuweza kuamini ni pale Mh. Rais alipokuwa anataja wasanii wakubwa mbali mbali akiwemo, Ludacris,Trey Sings, Lil Wayne, Usher Raymond na wengine wengi tena pamoja na mameneja wao.
Mh.Raisi alizidi kufunguka kwa jinsi Diamond Platnumz alivyomfurahisha katika uwakilishi wake wa tuzo za Mtv “Nilikutana na Diamond Nje ya nchi, nikamkaribisha lunch akaniambia amekuwa nominated kwenye tuzo za MAMA na za BET, nimeangalia MAMA, Diamond hakushinda ila aliperform vizuri sana na watu wakamfurahia sana”- alifunguka Mh.Raisi. Nadhani hakutakuwa kutokea na Raisikama huyu mwenye kujua mambo mengi kuhusu sanaa, ni raisi wa kipekee ambaye anafaa hata kuwa meneja wa wasanii.
0 comments:
Post a Comment