Kupitia Ukurasa wake wa INSTAGRAM..Mtangazaji wa Clouds FM, DIVA atoa ushauri huu kwa wasanii wa hapa TZ....Nanukuu.. "Goodmorning Tanzania. So kuna Mtu aliniuliza kwanini Nigeria wanakuwa wameishika Africa na kuwa nominated kwenye Tuzo nyingi Africa na duniani kwa ujumla. Kwanza ifahamike Nigeria kuna watu zaidi ya Mil170 na Tanzania ni kama watu Mil44 hivi kwa harakaharaka na hatutaweza hata robo kushindana nao sababu hawa jamaa kwanza wanashinda katika internet. Watumiaji wa Internet Tanzania ni asilimia haizidi 4 au 5. Hatufiki watu mil1 na nusu na wengi wanaotumia wako nje ya Tanzania na Miji Mikubwa sana. Ndio maana kama una biashara yako ya maana Tangaza radioni sababu watu mil44 wote karibia wana Access ya radio. Mtu yoyote afanyaye kazi kwenye media ni Maarufu zaidi ya hawa wa instagram facebook au twitter au bloggerz au wanaomiliki blogs. Sababu hao watu mil44 ni lazima watamfahamu tu. Pili uki shoot video na Jamaa wa Nigeria wanaichukua na kukutambulisha duniani wenyewe kupitia ile pesa yako na sio kuwa wewe ndio eti unasumbuka hapana. Na sio kuwa ukichaguliwa BET au sijui wapu ni Nguvu zako hapana ni hao Jamaa wanafanya hayo yote. Nawashauri Wasanii wenye uwezo wa kufanya video na watu wa Nigeria wafanye hivyo na Matunda yao watayaona. They gon make you famous Hutaamini. Wanasambaza kazi zako wenyewe kupitia Pesa yako uliolipa wakati una shoot video. Adam Juma did it Mwanzo pia...so Nashauri wa Tanzania tuwekeza katika video Nje za Nchi kama unataka Kutangaza nchi na kuchaguliwa kwenye awards kubwa duniani. Nigeria pia Elimu inachangia. Hawa watu wanaongoza kwa mengi duniani ikiwemo wizi wa ki electroniki pia. So ndio maana wanashinda ma tuzo ma nini....akili nyingi....degree na masterz kibao huko. Wasanii Tanzania pia ongezeni Elimu zenu itawasaidia zaidi </div>
.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment