Beyonce Knowles alipata tatizo la aina yake alipowasapraiz mashabiki wake kwa kuungana jukwaani na mumewe Jay Z ghafla katika Global Citizen Festival iliyofanyika wikendi iliyopita.
Akiwa katika harakati za kuimba na kucheza, ghafla top yake nyeupe iliafunguka na kifua chake kubaki wazi huku ‘maziwa’ yakitoka nje ya bra iliyokuwa na rangi ya ngozi yake.
Hata hivyo, kitendo hicho kilifanyika ndani ya sekunde chache kiasi kwamba mashabiki waliokuwa wanashangweka hawakukishtukia hadi pale video ya show hiyo ilipotoka na wana habari wakacapture picha na hivi sasa imesambaa.
0 comments:
Post a Comment