kwa mujibu wa TMZ, Amber Rose alichukua uamuzi huo baada ya kumfumania Wiz Khalifa akiwa na mwanamke mwingine nyumbani kwake majira ya saa nane usiku.
Taarifa hizo zimeunganishwa na tweet ya Amber Rose inayoeleza kuwa anaendelea kulikumbuka tukio hilo.
Hata hivyo chanzo cha karibu na Wiz Khalifa kiliieleza TMZ kuwa rapper huyo aliwaambia kuwa alifanya makusudi kwa kuwa hataki tena kuendelea kuwa mume wa Amber Rose.
“I just didn't want to be married to her anymore.” Chanzo hicho kimemkariri Wiz Khalifa.
Inaelezwa kuwa hii ni moja kati ya sababu zilizomfanya Wiz Khalifa kutopinga uamuzi wa Amber Rose kudai talaka yake.
Taarifa za awali zilieleza kuwa Amber Rose na Nick Cannon walianzisha uhusiano wa mapenzi na kuwala kisogo Wiz na Mariah Carey lakini wote walikanusha taarifa hizo.
0 comments:
Post a Comment