Waandaaji wa shindano la Big Brother Africa, kampuni ya M-Net na Endemol SA wametoa tamko jipya leo kufuatia kuungua kwa jumba lililotumika kuendeshea misimu iliyopita.
Katika tamko hilo, waandaaji hao wameeleza kuwa shindano hilo litafanyika kama lilivyopangwa na kwamba tayari wameshapata jumba jingine katika eneo lingine duniani.
“M-Net na Endemol SA wametumia masaa 48 kutafuta eneo nyumbani na hata katika nchi za kimataifa ambapo msimu wa 9 wa reality show maarufu Afrika utafanyika.
“Baada ya kutafuta namna zote, timu inayofuraha kutangaza kuwa show itaendelea kwa kuwa sehemu imeshapatikana kuhakikisha show inaenda hewani ndani ya mwezi ujao.” Wameeleza katika tamko lao.
Wamewashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao wakati wa siku mbili za wasiwasi baada ya kuungua kwa jumba hilo.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaamini kwamba tukio hilo lilitengenezwa na waandaaji hao kwa lengo la kuvuta umakini zaidi aka ‘kiki’ kwa lengo la kuunogesha msimu huu uliopewa jina la ‘Hot Shots’.
0 comments:
Post a Comment