Wakati dunia ukiuchukua mtandao wa Facebook kama mtandao wa kijamii wenye watu wengi na uliosambaa zaidi duniani, mtandao huo umepata mpinzani mkubwa ambaye anachukuliwa na wengi kama mbadala wake, ‘Ello’.
Mtandao wa Ello uliotengenezwa na Paul Budnitz umetimiza wiki nane tu tangu uanze kutumika na maelfu ya watu wameendelea kujiunga ndani ya muda mfupi.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wameukosoa mtandao wa Facebook kuwa sio mtandao bora wa kijamii na kwamba umejikita zaidi katika kufanya biashara kupitia matangazo tofauti na ilivyo kwa ‘Ello’ ambao haulipishi kiasi chochote cha fedha kwa matangazo.
Mwanzilishi wa Ello amekaririwa akisema kuwa anaona Facebook kama mtandao uliojikita zaidi kwenye kufanya matangazo badala ya kuwa mtandao wa kijamii.
Mtandao huo umebatizwa jina la ‘Anti-Facebook’.
“Kila kitu kiko kwenye mpangilio mzuri wa mfuatano. Watu wataona kile tu wanachotaka kuona.” Amesema muanzishi wa Ello, Budnitz.
0 comments:
Post a Comment