Kuanzia jumatatu ijayo kupitia account zake za mitandao ya kijamii facebook
titwer na instagram @ommydimpoz atakua anaendesha shindano la kucheza wimbo huo, shindano alilolipa jina "Lima na Tupogo" ambapo kila mwisho wa wiki mshindi
atazawadiwa mtonyo laki 5 cash kutoka mfukoni kwa Ommy dimpoz.
Lima na tupogo ni moja kati ya vionjo kwenye Tupogo,
sasa kwasababu mafans wetu wanatuweka hapa na wanatufanya tuwe hapa na
wanatupa nguvu ya kufanya kazi zaidi kwahiyo nimeona hii wakati nimetoa
hii video ya tupogo, na kama kuwataka radhi hizi kwasababu uanajua
tupogo ni video ambayo ingetakiwa kutoka mda mrefu ndio maana nikaamua
nifanye remix na niitolee video, ambayo itakuwa ni kama bonus track
katika album yangu ambayo itatoka siku ya Valentines.....
Lima
na Tupogo ni style ambayo nimewapa nafasi mashabiki wa PKP kutumia
nafasi hii kulima lima lima lima, wanakuwa wanalima halafu mshindi kwa
kila wiki anaondoka na laki tano na tutakuwa na wiki nne,.....Ili
kushiriki kutakuwa na hashtag ya Lima na Tupogo ambayo
tutakuwa tunaweka clip kwenye acc yangu ya instagram facebook na twitter
kwahiyo tutakuwa tunafanya kwa kupitia social network kui-promote hiyo Lima na Tupogo na wengine kama wataweza ku-upload youtube
0 comments:
Post a Comment