Drama bado inaendelea! Mapenzi kati ya mastaa wawili Selena Gomez na Justin Bieber yameendelea kuwa kivutio kwa mashabiki wao na safari hii baada ya kuwepo na taarifa za kuachana kwao,Gomez amefunguka na kusema licha ya kutokuwa pamoja bado anampenda Bierber.
Gomez mwenye miaka 22 alipohojiwa jana alisema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mtu na hakuna kibaya kati yake na mwimbaji huyo,ingawa amekiri wana historia ya kuachana na kurudiana mara kwa mara kwa miaka minne sasa.
“”Nilikua ninamuheshimu na kumpenda”…Gomez aliiambia redio NRJ ya nchini Norway wakati alipohojiwa kuhusu wimbo wake mpya wa ujulikanao kama ‘Hearts wants what it wants’ ambao umeonekana kama umelenga kumuhamasisha Bieber ili warudiane.
0 comments:
Post a Comment