.
NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE ALIVYOMUANDALIA BALOZI MWANAIDI MAAJAR(FAREWELL PARTY) PARTY YA KUMUAGA
Gallery
Posted by kifesi |
Kitu kibaya zaidi kinachokosewa na wanadamu wa nyakati hizi kwenye mapenzi ni kwamba wanapingana na haja za nafsi zao na wanafuata msukumo wa matamanio ya viungo vyao vya uzazi,unapomuoa mwanamke kwa sifa ya kujua kukata mauno unakosea kwa kuwa si kila muda utahitaji kukatiwa viuno kwenye ndoa.
kuna kipindi utahitaji ukarimu wa mumeo wa mumeo ili uweze kufurahia maisha ya ndoa na pia kuna kipindi utahitaji tu busara za mkeo ili uweze kuikamilisha furaha yako kwenye ndoa.
Tunapochagua wenzi wetu wa maisha tusiangalie sababu za kimatamanio kwani vile vitu vilivyokuvuta kwake baada ya muda utaviona vya kawaida na utamuhitaji yeye kama yeye na sio sababu ya vile alivyo navyo na hapo ndipo yanapo simama mapenzi halisi kwa maana ya mapenzi na kamwe hawezi kuwa si size yako na wala hata kupwelepweta bure,kwani mapenzi yenu yenye nguvu yataziba kila mahala penye tundu ya usaliti.
\
Posted by kifesi |
Kwenye kila idara siku hizi kuna habari zake nyingi tu, utaambiwa Wanamichezo 10 matajiri duniani, 10 wanaouza zaidi kibiashara, Magari 10 ya bei ghali zaidi duniani…. hizo ni baadhi tu ya countdown ambazo tunazo kwenye haya maisha ya kila siku.
List ya hawa warembo ilitoka zaidi ya miezi miwili iliyopita so kama ilikupita fanya hesabu pamoja na mimi kwenye hii post, wanasema sio Warembo wa Ulaya bali hii ni list ya dunia.
#1 Nina Dobrev - mrembo huyu aliyetajwa kushika namba moja ni mwigizaji na Model mzaliwa wa Bulgaria aliyekulia Canada.
#2 Emmanuelle Chriqui – Ni mwigizaji raia wa Canada ambaye alianza uigizaji akiwa na miaka 10 ambapo jina lake linahusika pia kwenye movie ya mwaka 2008 ‘You Don’t Mess with the Zohan’
#3 Jessica Alba – Ni mwigizaji kutoka Marekani ambae ni mfanyabiashara na model pia ambapo alianza uigizaji akiwa na umri wa miaka 13 tu.
#5 Monica Bellucci – Mrembo huyu wa Italy ndio kashika namba 5, akiwa ni mwigizaji pamoja na fashion Model.
#6 Olivia Wilde – Olivia ni mwigizaji wa Marekani, screenwriter na producer vilevile na pia amewahi kuonekana kwenye movie ya ‘The Girl Next Door‘
#7 Scarlett Johansson – ni Mmarekani ambae ni model, mwigizaji na mwimbaji pia aliyezaliwa kwenye jiji la New York.
#10 Angelina Jolie – Namba kumi ndio hii imechukuliwa na Angelina ambae ni mwigizaji na mwogozaji wa Filamu.
Posted by kifesi |
Imeripotiwa kuwa Miss Tanzania wa zamani ambae ni mchumba wa mda mlefu wa billionea reginald mengi, jackuline klyn leo amefanikisha kufunga ndoa huko ufaransa paris na billionea huyo, kama ilivyo ada na kuwaida mitandao ya kijamii ukiwemo na insta, as it known yakuwa hapo juzi kati mwanadada huyo aliweka tiza kwenye mtandao wake wa insta ya kuwa final destination, so kama ulikuwa hujui ndo tunakufungua macho yakuwa final destination yenyew ndio hii ya kuolewa baada ya kupitia misukosuko mengi, soon tutawaletea picha za harusi na ndoa ya klyn,na mengi huko france
by thechoicetz
Posted by kifesi |
Diamond anapigwa vita sana adondoke, ila tusichojua wabongo ni kuwa Diamond akidondoka mziki wetu unadondoka pia Dee ametuweka kwenye ramani ya muziki ambayo hatukuifikiria kwa miaka ya karibuni kwa juhudi zake, ila sisi badala ya kum-support ndio kwanza tunampiga mawe hatari. Kuna nchi kibao hapa Africa kitu kizuri pekee wanachojua kutoka bongo ni Diamond na ushiriki wetu Big brother.
kila nikiskia kapiga hatua flani nafarijika kama Mtanzania na namuheshimu.
Ila sio issue,kama tunaona ni sawa kumshusha tumshushe tu halafu tuanze upya kuwapandisha tunaowapenda, tukishindwa tuanze kulaumu jinsi Nigeria walivyo-dominate game, si ndio zetu.
kila nikiskia kapiga hatua flani nafarijika kama Mtanzania na namuheshimu.
Ila sio issue,kama tunaona ni sawa kumshusha tumshushe tu halafu tuanze upya kuwapandisha tunaowapenda, tukishindwa tuanze kulaumu jinsi Nigeria walivyo-dominate game, si ndio zetu.
Posted by kifesi |
Msanii Diamond Platnumz amepost moja ya nyumba yake akisema hiyo ni moja ya kumi ya nyumba alizonazo, huku akisema ina vitu kama gym, jaccuzi,swimming pool, studio, pooltable, lounge etc
Reply
Posted by kifesi |
Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu Bobbi Christina adondoke bafuni na kupoteza fahamu, japo familia yake imekuwa ikitoa taarifa kwamba hali yake inaendelea vizuri zipo taarifa zinazosema kuwa hakuna dalili yoyote ya msichana huyo kupata nafuu.
Familia yake, watu wa karibu wamekua wakitumia muda mwingi kumfanyia maombi msichana huyo.
Familia yake imepanga kukutana mwishoni wa wiki hii ili kuzungumzia hali ya msichana huyo ambaye mpaka sasa anatumia mashine kupumua na huenda wakafanya uamuzi wa wa kumtoa kutoka kwenye mashine hiyo ya kupumulia.
Bibi wa Christine ambaye ni mama mzazi wa Whitney Houston, amesema ni bora mjukuu wake akatolewa mashine hiyo, baba yake mzazi Bobbi Brown ni kama yuko njiapanda juu ya nini aamue.
Kwa mujibu wa daktari anayesimamia matiibabu ya binti huyo amesema hadi sasa hakuna dalili yoyote ya matumaini ambayo Bobbi Christina ameonesha tangu alazwe hospitalini hapo.
Posted by kifesi |
Akiwa na miaka 17 tu mdogo wake Kim Kardashian ‘Kylie Jenner’ ameanza kufanya photo shoot tofauti. Hii amefanya huko Hollywood Hills jumanne ya wiki hii.
Lakini pia Wiki iliyopita mpenzi wake ambaye ni rapa Tyga ’25’ alithibitisha kuwa ni wapenzi na Kylie kwa kuweka picha ya Kylie iliyoambatana na ujumbe wa “Certain things catch your eye, but only few capture the heart.”
Posted by kifesi |
Daktari mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni mgonjwa aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa utoto wake.
Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa kuzungumzia tabia za Shilole za kugombana mara kwa mara na mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia linalomsumbua mmoja wao au ni ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.
“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa unyanyasaji akiwa mtoto ‘child abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa, kupigwa, kunyimwa chakula au mateso ya aina hiyo, akikua bila kupata tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu mzima.
“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kupenda kujitenga, hasira za karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni kumfanyia mtu mwingine hasa mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu wanaita ‘Propensity Victimization,’” alisema daktari huyo.
Alisema katika nchi zilizoendelea, tatizo hilo hupewa kipaumbele katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika kwani madhara yake huwa ni pamoja na mwathirika kuamua kujinyonga au kuua.
Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana kufanana na matukio yaliyowahi kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa miaka 14, aliwahi kubakwa, pia anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu wenye umri mkubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri mdogo.
Subscribe to:
Posts (Atom)