Kwenye Leo Tena alikuwepo Diamond Platnumz pamoja na meneja wake, Babu Tale.. kama kawaida ya show ya Leo Tena pale huwa ni story nyingi nyingi zinakuwa zinaendelea, lakini Diamond nae akashea na watu wake kuhusu HEKAHEKA aliyowahi kukutana nayo.
Kulikuwa na maswali pia ambayo ilibidi Diamond ayajibu, mengi yalitoka kwa wasikilizaji wa show hiyo.
Ikaulizwa kuhusu tetesi za yeye na Meneja wake Said Fella kuwa na ugomvi, kisa vijana wa Yamoto Band hawajanunuliwa magari? Jibu la Diamond ni hapana.. hakuna ugomvi wowote, Babu Tale akasema mipango ya Management yao ni kufanya mengi mazuri kwa vijana wa Yamoto Band.. HAKUNA UGOMVI!
Likatupiwa swali la umri wa mpenzi wake Zari je? akajibu kwamba ni miaka 34 tu.
Ikaja sasa time ya kusikiliza Hekaheka aliyowahi kukutana nayo wakati anaanza muziki.. amesema alikuwa anapenda sana kuimba wimbo wa Z Anto wa ‘Binti Kiziwi’ .. wengine waliamini yeye ndio Z Anto mwenyewe, ikatokea msichana akampenda akijua anayempenda ni Z Anto.. baada ya video ya Z Anto kutoka watu wakamjua kwamba sio yeye ilibidi asiendelee kukatisha maeneo hayo.
Wengine waliuliza kama wimbo wa ‘Nasema Nawe’ ni wimbo alioimbiwa mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu.. nalo Diamond kalijibu, amesema huo wimbo hajaimbiwaWema.. Ila aliuimba wakati akiwa na Wema… Hiyo ni burudani ambayo imezoeleka na wanawake wa uswahilini kwa hiyo kaona nao awaimbie.
Amekataa kuwa na ugomvi wowote na Ommy Dimpoz, na wala hajawahi kukutana naWema tangu walipoachana.
Kuhusu ujauzito wa Zari, Diamond amesema anatarajia mtoto mwezi wa saba au wa nane hivi.
Utayasikiliza yote hayo hapa chini mtu wangu, play..
0 comments:
Post a Comment