Weekend iliyopita Escape One kulifanyika show iliyowakutanisha mastar wakubwa ndani na nje ya TZ kama Christian Bella, Ruby,Ali Kiba, Kassim Mganga, Ommy Dimpoz, Msami, na Kenya.. WOTE kwenye stage moja watu wakaenjoy pamoja mtu wangu..
Katika tukio lililowashangaza wengi ni ishu ya msanii Ommy Dimpoz alipojikuta akishindwa kujizuia mbele ya mashabiki zake na kuanza kulia wakati akiimbi wimbo wa ‘Nani kama mama‘ alioshirikishwa na Christian Bellakitendo kilichomfanya ashindwe kuendelea kuimba na kushuka jukwaani.
Soudy Brown alikuwa eneo hilo na kuamua kuzungumza nae kutaka kujua tatizo ni nini… Dimpoz amesema aliandika wimbo huo kwasababu ya kumbukumbu ya kifo cha mama yake aliyefarika miaka 15 iliyopita na kumuacha akiwa mdogo.. wakati anaimba wimbo huo kulimfanya akumbuke mapenzi ya mama na kutamani kama mama yake angekuwepo na kuona mafanikio ya mtoto wake akiwa mtoto pekee.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza stori yote…
crdt:mmillardayo
0 comments:
Post a Comment