Ijumaa hii Wema Sepetu alikuwa mgeni kwenye kipindi cha Ubaoni cha EFM. Miongoni mwa mambo aliyoulizwa ni pamoja maisha baada ya kuachana na Diamond Platnumz.
Haya ni mambo 10 aliyosema:
1. Maisha yake bila Diamond yako poa tu japo mazoea yaliyokuwa yamezidi kati yao yanamfanya wakati mwingine kummiss!
2. Ameshakubali ukweli kwamba yuko mbali na Diamond
3. Anaamini kuwa Diamond anammiss pia kutokana mazoea waliyokuwa nayo
4. Wema na Diamond sio marafiki
5. Hana kinyongo na Diamond ila anaamini kuwa Diamond bado ana kinyongo naye
6. Ni shabiki na ataendelea kuwa shabiki wa nyimbo za Diamond
7. Hawajahi kukutana na Diamond tangu waachane
8. Hajawahi kumpigia simu
9. Aliwahi kumtumia meseji Diamond kumpa pole kwa kuuguliwa na mama yake
10. Bado hajapata mwanaume mwingine
0 comments:
Post a Comment