Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kwamba idadi ya wanawake wasiyoikubali miili yao hapa nchini ni kati ya 25 hadi 35, kwa maana kwamba ni wanawake 25 hadi 35 katika kila wanawake 100 wasiyokubali miili yao. Ndiyo maana siku hizi tunashuhudia baadhi ya wanawake hapa nchini wanaohangaikam kutafuta dawa za kukuza makalio yao na kubadili rangi ya ngozi zao. Kuna yale ambayo mtu hawezi kuyabadili, kama vile sura, makalio, kimo na maumbile ya sehemu za siri. Hata hivyo baadhi yake, huwa yanabadilishwa kwa kufanyiwa upasuaji na matumizi ya
dawa au kemikali fulani. Lakini siku zote mabadiliko hayo yemekuwa ni maumivu makubwa kwa wanaoyafanya, lakini pia ni gharama. Kumbuka wale ambao wamebadili matiti yao kuwa makubwa au madogo wamejikuta wakilipia gharama kubwa ya maumivu ya kihisia, kwa matiti hayo kuwa kama mawe tu kwa kukosa msisimko yanapoguswa. kila mtoto hufundishwa kama ajikubali au ajikatae wakati anapokua. Mtoto anapooneshwa kwamba, ana mwili mzuri au anapooneshwa kwamba, ana sura nzuri na ana uwezo mkubwa kiakili, hukua akimini hivyo. Anapooneshwa kinyume chake, huamini hivyo pia. kumbuka kwamba, siku hizi kuna walezi au wazazi wengi. Kuna televisheni, inteneti, vijarida na redio ambavyo vyote kwa pamoja humfundisha mtoto kuwa yeye ni nani. Kwa mtoto wa kike kama atawatazama akina Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange au Wema Sepetu anaweza kuamini kwamba, mwanamke mrembo anayekubalika kwa viwango vya urembo ni yule mweupe mwenye umbo namba nane na mwenye makalio makubwa yaliyobinuka kama hao wasanii niliowataja hapo juu. Masogange Kwa hiyo mtoto wa kike ataanza kuchanganyikiwa akishagundua kwamba muonekano wake haufanani na hao wasanii niliowataja, hata kama nyumbani alifundishwa kwamba mwili ni mwili na ule mtu alio nao ndiyo wake. Lakini, kama hakupata bahati hiyo, hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi. Kwa hiyo bado kama wazazi inabidi tufanye kazi ya ziada kuwaambia mabinti zetu kwamba, wana miili mizuri na wenyewe ni wa zuri bila kujali wana muonekano wa namna gani.
0 comments:
Post a Comment