Kaingia kwenye HEADLINES za Magazine kubwa duniani, BLACK ENTERPRISE ambao wamefanya nae exclusive interview, mengi kayasema hapa mengine hata sikuwahi kuyajua kutoka kwake.. kumbe ishu ya kuingia kushiriki Miss Universe hata hakuwa na idea ya kitu anachokifanya, aliingia kwa kujifurahisha tu !!
Kingine alichokiongea ni ishu ya Flaviana Matata Foundation, taasisi ambayo aliianzisha kwa ajili ya kusaidia wasichana yatima kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mahitaji muhimu ya Shule.
“Niliwahi kumuona marehemu mama yangu akisaidia watoto wengine kuwapeleka shule.. Nilikuwa mdogo sana lakini alikuwa akituambia na ndugu zangu umuhimu wa kusaidia watu ambao wanahitaji msaada.. Nilianzisha FMF kwa ajili ya kuendeleza moyo wake wa kujitolea..“– Flaviana Matata.
“Jitihada nnazozifanya kusaidia wasichana kupata elimu itakuwa ni kitu ambacho kila mtu anaweza kukipongeza..“– Flaviana Matata.
0 comments:
Post a Comment